Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, ametuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma kutokana na kifo cha Kocha Msaidizi wa Majengo Queens ya Singida, Godfrey Gwitaba.

Kadhalika Rais Karia ametuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Singida, Mhe. Mussa Sima kutokana na kifo cha kocha huyo kilichotokea leo Desemba 5, mwaka huu mjini Singida.

Salamu hizo za rambirambi pia zimekwenda kwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo ya Singida ambayo iko Arusha ikishiriki ligi ya wanawake hatua ya makundi. Iko kundi B.

Rais Karia ametaka wanafamilia hao pamoja na ndugu, jamaa, marafiki, majirani kuwa na moyo wa subira wakati huu wa kipindi kigumu cha msiba wa Gwitaba.

Bwana ametoa Bwana amtwaa. Jina la Bwana lihimidiwe.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.