Droo ya 8 bora ya NBC U 20 yaweka wazi makundi

    Droo hiyo ya Ligi ya NBC ya vijana (NBC Youth League 25/26) imefanyika Juni 9, 2026 makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) jijini Dar es Salaam.

    Kundi A linaundwa na mabingwa mara nyingi wa ligi hiyo Mtibwa Sugar pamoja na Young Africans, Mashujaa FC na Mbeya City.

    Kundi B lenyewe zipo timu za Azam FC, Dodoma jiji, Simba SC na JKT Tanzania.

    Mashindano hayo yanayofanyika kwa msimu wa nane mfululizo yanatarajia kuanza tarehe 18 Juni 2026 kwa mechi za kundi A.

    Mechi za kundi B zitachezwa 19 Juni 2026 kabla timu hizo hazijakwenda kwenye hatua nyingine.

    Pia mechi hizo zinatarajiwa kutamatishwa kwa Fainali ambayo imepangwa kuchezwa tarehe 1 mwezi Julai.

    Akizungumza baada ya droo hiyo, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto amezitaka klabu kuzingatia sheria na taratibu za ligi hasa kwa upande wachezaji (vijana) wanaokidhi kushiriki kwa utambulisho wa leseni.

    “Nitoe rai kwa makocha kuzingatia wachezaji wanaokidhi kwenye usajili, wale wenye leseni kama ilivyokuwa kwenye hatua za awali.

    “Makocha wametaka muda mwingi wa mapumziko na maandalizi kuelekea kwenye kila mechi, hivyo tumeangalia hilo zaidi kwenye upangaji wetu wa ratiba,” alisema Kizuguto.

    Mechi zote zitapigwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

    Share.