Wasichana U-17 Tizi kwa Kwenda Mbele
Timu ya Taifa ya wasichana chini ya miaka 17 imejipanga vyema kuendeleza ushindi kwenye mchezo wake wa marudiano dhidi ya Botswana mara baada ya kupata ushindi wa mabao 7-0 kwenye mchezo wa awali uliochezwa Machi 06, 2022 kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar.
Timu hiyo ambayo imeendelea na kambi huko visiwani Zanzibar imekuwa ikipiga tizi la nguvu ilihali katika kujiweka sawa kuendeleza ushindi na hatimaye kufikia malengo ya kutinga kwenye hatua ya robo Fainali huku ikiwa na malengo mengine makubwa zaidi ya kufika mbali kwenye mashindano hayo.
Kwa mujibu wa maelezo ya kocha mkuu Bakari Shime alisema kuwa kikosi kimeendelea na kambi na timu itaondokea huko kuelekea nchini Botswana kwaajili ya mchezo wa marudiano, na kwamba kwa upande wao mechi ndio inaanza kwani ushindi wa awali haumaanishi kushinda pia mechi ya pili. Hivyo wameendelea na maandalizi ili kuweza kutetea ushindi walio nao.
“kwetu mechi ya marudiano ni sehemu ya maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Burundi kufuatia kujitoa kwa mpinzani wa Burundi hivyo anamsubiri mshindi kati ya Tanzania na Botswana, na mpaka sasa timu yetu inauhakika wa takribani 60% kuweza kufika katika hatua inayofuata”. Alisema hivyo
Mchezo wa marudiano utachezwa Machi 20, 2022 huko Botswana ukiwa ni mchezo wa pili kwa timu hizo kwenye hatua ya kwanza ya makundi.Fainali za kombe la Dunia kwa wanawake 2022 zitafanyika mwaka huu nchini India.