Barka Atinga Kukipiga Ulaya
Kijana wa Kitanzania aitwae Barka Seif Mpanda (7) leo Agosti 28, 2021 ametua katika kituo cha Ajax Amsterdam Academy,
kilichopo nchini Uholanzi kwa ajili ya kuanza majaribio.
Kijana huyo mwenye kipaji cha aina yake amekwenda nchini Uholanza kwa ajili ya kufanyiwa Majaribio kwenye timu za mpira wa miguu za watoto
Barka anaweka historia ya kuwa kijana wa kwanza wa Kitanzania kufanya majaribio katika kituo hicho maarufu duniani katika kuwapika vijana wadogo kisoka.
Akiwa Ajax Amsterdam Academy, Kijana Barka atafanya majaribio kwa muda wa wiki mbili ndani ya kituo hicho maarufu duniani.
Kutokana na uwezo mkubwa ambao amekuwa akiuonesha katika kusakata kandanda unaochagizwa na kipaji alichonacho kuna uwezekano mkubwa Barka akafuzu majaribio hayo; hivyo kuandika rekodi nyingine tena kwa Tanzania kutoa kijana mdogo kwenda kujiunga na moja kati ya vituo vikubwa vya soka duniani.
Kijana Barka historia yake kwa Tanzania anatokea katika kituo cha michezo kinachojulikana kwa jina la Magnet Academy.
Barka Seif anaungana na baadhi ya wachezaji maarufu waliowahi kupita katika kituo hicho ambao ni; Frank Rijkaard, Frank de Boer, Clarence Seedorg, Patrick Kluivert, Dennis Bergkamp, Marco Van Basten na Edgar Davis.
Endapo kijana huyo atafanikiwa kufuzu na kuteuliwa kujiunga kwenye kituo hicho atazidi kuendelea kuitangaza vema Tanzania kisoka hasa katika anga za Kimataifa, huku Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania nalo likijipatia sifa kwa usimamizi na uhamasishaji Mzuri wa maendeleo ya soka la vijana nchini.