CAF Yaumwagia Sifa Uongozi na Utawala Bora wa Karia

Uongozi na utawala bora uliopo chini ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia umezidi kuthibitika wazi kwa mafanikio makubwa ambayo hakuna haja ya kusimuliwa ili kuweza kuyafahamu bali kwa kujionea mambo makubwa aliyokuwa akiyafanya na kuendelea kuyafanya katika kuhakikisha soka lina zidi kukua nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe 13 Agosti, 2021 alipokwenda kutembelea moja kati ya miradi mikubwa ya inayoendelea kujengwa inayohusisha ujenzi wa vituo vya kuvumbua, kuibua na kukuza vipaji vya vijana kwenye mchezo wa mpira wa miguu kuanzia kwa vijana wadogo wenye umri chini ya miaka 9, 11, 13, 15, na kuendelea; mradi unaosimamiwa na TFF wakiongezewa nguvu kubwa kutoka FIFA.

Rais Motsepe alisema kuwa amefurahi na anajivunia kuona mambo makubwa na mazuri ya maendeleo kwenye mpira wa miguu yanayo fanywa na Rais Wallace Karia katika kuhakikisha soka linazidi kukua nchini na hata Afrika kwa ujumla.

Alipongeza pia utekelezaji mzuri wa majukumu kwa uongozi wa TFF akisema kuwa katika kila uongozi mzuri hapana shaka mafanikio lazima yawepo huku akisisitiza kulingana na utendaji huo  mchezo wa mpira wa miguu wa Tanzania (Wanawake na Wanaume) utakuwa kwa kiwango kikubwa kwa Afrika na hata pengine kupiga hatua kubwa zaidi kuwa bora kwa ngazi ya Dunia.

Aidha, amemshukuru Katibu Mkuu wa CAF Veron Mosengo kwa kushirikiana bega kwa bega na uongozi wa TFF katika kulitimiza jambo hilo kwani amekuwa akishirikiana nao tangu likiwa wazo mpaka kufikia hatua ya kumalizika kwa miradi hiyo.  Katibu huyo aliongeza kwa kusema kuwa uongozi wa CAF wanajivunia kuona hatua kubwa ya maendeleo ambayo TFF wanazidi kupiga katika soka.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa(BMT) na aliyekuwa Rais mstaafu wa heshima TFF, ndugu Leodgar Tenga alisema kuwa  imekuwa ni bahati kupata wageni kutoka CAF kuweza kushuhudia nao kwa pamoja mradi huo ambao wamekuwa wakiweka nguvu katika kuhakikisha malengo ya TFF yanatimia; amempongeza pia Rais Karia na kamati yake kwa utendaji mzuri na wauwazi.

Akitoa shukrani mbele ya viongozi hao wakuu katika soka Barani Afrika Rais Wallace Karia amefurahi kupokea ugeni mkubwa kutoka CAF na BMT akisema kuwa amefurahi kwa jambo hilo la Rais wa CAF  ambaye pia ni makamu wa Rais wa FIFA kuweza kutembelea mradi huo ambao umekuwa ukiendeshwa kwa pesa kutoka FIFA. Rais Karia alimshukuru pia Rais mstaafu wa TFF Leodgar Tenga akisema kuwa anamchango mkubwa katika upatikanaji wa maeneo yaliyo beba miradi hiyo hususani ule mradi uliopo jijini Tanga.

Viongozi waliotembelea mradi huo ni; Rais wa CAF Patrice Motsepe, Katibu Mkuu CAF Veron Wilfred,  Rais wa TFF Wallace Karia, Katibu Mkuu wa TFF Kidau Wilfred, Mwenyekiti wa BMT Leodgar Tenga pamoja na viongozi  na wadau wengine wa sok