RAIS KARIA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA VIENNA, AISHUKURU FIFA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ametoa shukrani kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa washiriki wa Warsha ya kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu duniani inayohusisha Nchi Wanachama wa UEFA na CAF inayoendelea Vienna, Austria.

Rais Karia amesema ni heshima kwake na shirikisho kushiriki pamoja na mashirikisho mengine kutoka Afrika na Ulaya.

“Ni furaha kuwa miongoni mwa washiriki kwasababu mijadala mingi inasaidia sana na inatupa data za kuweza kuendeleza mpira wa miguu Nchini kwetu”

Amesema kuna haja ya warsha za aina hiyo kuendelea kutolewa zaidi ili kupata maarifa yanayoweza kusaidia katika shughuli za kila siku katika maendeleo ya mpira wa miguu.

Nchi zinazohudhuria kwenye Warsha hiyo ni Finland, Moldova, Wales, Austria, Georgia kutoka UEFA na Gabon, Morocco, Senegal, Tanzania na Cameroon kutoka CAF