Fainali ya michuano ya CECAFA U23 msimu wa 2021 imerindima hii leo Julai 30, 2021 kwa kuzikutanisha Tanzania U23 dhidi ya Burundi U23 katika uwanja wa Bahir Dar, Ethiopia moja kati ya mchezo uliokuwa ukisubiriwa na watu wengi sana.
Timu zote zilingia uwanjani kwa hali ya kushindana huku kila moja akijilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza licha ya hali ya mvua na baridi kali katika mji wa Bahir Dar lakini soka safi lilionekana na kufanya kipindi cha kwanza cha mchezo huu kumalizika kwa matokeo ya 0-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kidogo vijana wa Tanzania U23 walijaribu kufika zaidi zangoni mwa Burundi U23 na kukabia kwanzia juu lakini haikusaidia mpaka dakika 90 mchezo ukamalizika kwa matokeo ya 0-0 hivyo mikwaju ya penati ikapigwa na Tanzania U23 wakaibuka na ushindi wa penati 6 kwa 5 na kufanya kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wa CECAFA U23 kwa mwaka 2021, Ethiopia.
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) na rais wa Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na Kati (CECAFA), Wallace Karia alitoa kongole nyingi kwa vijana kwa kujituma kwa hali na mali kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika michuano hii licha ya maandalizi mafupi lakini wamezidi kudhihilisha wao ni bora sana matokeo haya ni matunda yanayoletwa na maandalizi mazuri kwenye timu zetu za vijana kwanzia chini kabisa kwani vingi wao wametoka katika timu hizo.
Sambamba na hayo alishukuru sana serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa huwa sambamba na timu katika kila hatuwa baadhi ya viongozi waliwapigia simu wachezaji kambini na kuwapa moyo na anamini ushindi huu ni wa Taifa kwa ujumla kila mtu ana haki ya hushangilia na kujidani kwani mataifa yalikuwa mengi lakini Tanzania pekee ndio imeibuka bingwa sio jambo jepesi hata kidogo na kumalizia ushindi huu ni zawadi maalumu kwajili ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh, Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wa Makamu wa kwanza wa rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Athuman Nyamlani alisema “Maombi na baraka za watanzania ndio zimepelekea mpaka leo tunasherekea hivi na kuibuka na ubingwa lakini pia jitiada za kila mtu katika timu ndio chachu kubwa huku akitaka wadau mbalimbali kuwekeza kwenye soka la vijana kwa nguvu kubwa zaidi ya hivi sana kwani matunda yake ni makubwa kwa afya ya soka letu” alisema Nyamlani.