TFF Mabingwa Wapya Kombe la TFF Media Bonanza 2021

TFF yatwaa ubingwa wa bonanza la vyombo vya habari lililo fanyika Disemba 12, 2021 Gwambina Lounge kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe ambapo lililomalizika kwa timu ya TFF kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Global Group.

Bonanza hilo lililoanza kwa kupigwa mechi nane ambapo lilijumuisha timu 16 zilizoshiriki huku wengine wakiondolewa mapema kwenye mashindino na kuwaacha walio na nafasi ya kuendelea mbele kulingana na alama na matokeo waliyoyapata baada ya hatua hiyo, kwani kila timu ilipata nafasi ya kucheza mechi moja pekee ya kuamua hatma.

Mambo yaliendelea kuwa hivyo kwenye hatua ya robo fainali ambapo timu shiriki zilikuwa 8 zilizopita kutoka katika hatua ya 16 bora, kwenye hatua hiyo ni timu ya TFF pekee ndiyo ilipata nafasi ya kushinda bao moja la ushindi kunako dakika 90 za mchezo. Bao lilio wapatia tiketi ya kwenda hatua nyingine ya nusu fainali wakiwafunga Times FC huku wengine wakienda mpaka hatua ya kupiga mikwaju ya penati baada ya matokeo ya sare ndani ya dakika 90 ili kufuzu hatua ya nusu fainali.

Timu zilizo fuzu hatua ya nusu fainali ni; TFF iliyokutana na Clouds Media huku wakipata matokeo ya sare kwa kufungana bao 1-1, matokeo yaliyopelekea kupigwa mikwaju ya penati ambapo TFF walifankiwa kupata ushindi wa panati 5-4.

Mechi nyingine ya nusu fainali ilipigwa dhidi ya Global Group na Wasafi Media, hapo pia mambo hayakuwa rahisi kwa timu zote mbili baada ya kutoshana nguvu kwenye dakika 90 za mchezo hivyo kuamua mikwaju ya penati kupigwa ili kupata mshindi atakayekutana na TFF kwenye hatua ya Fainali ambapo matokeo yakawa na faida kwa Global aliyepachika wakipata penati 3 huku Wasafi ikipata penati 1 pekee.

Kwa matokeo hayo, hivyo hatua ya fainali iliwakutanisha TFF na Global Group wakiwa ndio wababe pekee walioweza kupenya mpaka hatua hiyo ya mwisho. Mechi hiyo pia ilikuwa kati ya mechi ngumu kupigwa kwenye hatua zote ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yalikuwa suluhu tasa.

TFF ilipata Ubingwa wa mashindano kwenye mchezo wa fainali kwa matokeo ya ushindi wa mabao ya penati 3-2 waliyoweza kupachika kimyani, huku Global Group wenyewe wakishika nafasi ya pili baada ya kupoteza kwa mikwaju ya penati katika mchezo huo wa fainali.

Timu zilizoshiriki kwenye “TFF Media Bonanza”; TFF, Azam Media, IPP Media, TBC, Clouds Media, Global Group, Wasafi Media, Mwanachi, Online Media, Dar 24, EFM, TSN, Times FM, Uhuru FC, Jamvi la Habari na African Media.

TFF Media Bonanza, ni tamasha lililo andaliwa na kuratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa lengo la kujenga na kudumisha mahusiano na vyombo mbalimbali vya habari nchini pamoja na wadau wengine wa soka ambao wamekuwa wakishirikiana kwa karibu. Tamasha hilo litakuwa likifanyika Disemba 12, ya kila mwaka.