Serengeti Girls yaondoshwa mbio za Kombe la Dunia

    Safari ya kufuzu Kombe la Dunia kwa timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imetamatika leo Mei 31, 2026 Uwanja wa Lucas Moripe baada ya kutoka suluhu na Afrika Kusini katika mechi ya marudiano.

    Kwa matokeo hayo Afrika Kusini inasonga mbele katika raundi ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia kwa jumla ya mabao 2-0 ambayo ilishinda katika mechi ya kwanza Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

    Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha wa Serengeti Girls, Bakari Shime alisema wamepoteza nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia lakini ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na timu yake.

    Tanzania ilianza safari yake ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kwa kucheza na Botswana ambapo ilipata ushindi wa jumla ya mabao 5-2. Raundi iliyofuata ndiyo ikadondokea kwa Afrika Kusini.

    Timu 24 zitashiriki Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia tarehe 17 Oktoba hadi Novemba 7 mwaka huu.

    Share.