‘Bado tuna nafasi mbele ya Afrika Kusini’
“Tumeona wanavyocheza, tumeona ubora wao. Walifanikiwa kutuweka kwenye shinikizo wakapata mabao, lakini mechi bado ipo.”
Ni kauli ya Kocha wa Serengeti Girls, Bakari Shime baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na Afrika Kusini (Bantwana).
Mechi hiyo ya raundi ya tatu kufuzu Kombe la Dunia 2026 imechezwa tarehe 23 Mei katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bao la kuongoza kwa Afrika Kusini lilifungwa na Khwezi khoza katika dakika ya tatu, la pili likifungwa na Aaliyah Jacobs dakika ya 24.
Akizungumza baada ya mechi Kocha Shime alisema wamepoteza mechi ya kwanza kwa idadi ndogo ya mabao, hivyo wanaweza kubadilisha matokeo katika mechi ya marudiano na kupata nafasi ya kuendelea katika raundi ya mwisho.
Mechi ya marudiano itachezwa tarehe 31 Mei nchini Afrika Kusini.

