Serengeti Girls yawasili Z’bar kuisubiri Afrika Kusini
Kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) kimewasili Zanzibar tayari kwa mechi ya raundi ya pili wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Afrika Kusini.
Serengeti Girls ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondosha Botswana kwa jumla ya mabao 6-2 huku Afrika Kusini wao wakifuzu moja kwa moja raundi ya pili baada ya Afrika ya Kati kujiondoa katika mbio za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia.
Jumla ya wachezaji 24 wamejumuishwa katika kikosi cha Serengeti Girls kitakachocheza mechi hiyo nyumbani na ugenini dhidi ya Afrika Kusini tarehe 23 na 31 Mei.
Wachezaji hao ni Nusrat Jaffar, Rhobi Daudi, Hadija Bakar, Janeth Matulanga, Asha Omary, Neema Mtunzi, Sunday Masasila, Elizabeth Chenge na Christer Bazil.
Wengine ni Fatuma Khamis, Helena Hamis, Yasinta Michael, Bahati Steven, Harrier Juma, Neema Thomas, Odilia Bakajibana, Eva Charles, Aneth Idama, Devotha Julius, Norah Mushi, Salima Ndaki, Anna Koku, Fatuma Aaron na Mary Mshana.

