Serengeti Girls kuivaa Afrika Kusini Mei 23

    Timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) inaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi ya raundi ya pili kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Afrika Kusini.

    Mechi hiyo itachezwa tarehe 23 Mei 2026 katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

    Ikiwa zimesalia siku tisa kabla ya mechi hiyo, kikosi cha Serengeti Girls kinachonolewa na Kocha Bakari Shime kimepiga kambi Kituo cha Ufundi cha TFF kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam kikiendelea kujiweka sawa.

    Akizungumzia maandalizi ya kikosi hicho, Kocha Shime alisema mechi hiyo itakuwa ngumu, lakini wamejipanga kuhakikisha wanacheza Fainali nchini Morocco.

    Serengeti Girls ilicheza Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka 2022 nchini India ambapo ilitolewa na Colombia katika hatua ya robo fainali.

    Share.