24 kuipigania Serengeti Boys AFCO

    TIMU ya Taifa ya wanaume chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) leo imeanza safari ya kwenda Morocco kwa ajili ya fainali za Afrika (AFCON) zitakazoanza tarehe 13 Mei.

    Serengeti Boys ambayo ipo chini ya Kocha Elieneza Nsanganzelu imesafiri na wachezaji 24.

    Kwa upande wa makipa ni Haji Abdalah, Abrahman Vuai na Rajabu Manyelezi.

    Mabeki ni Kassim Juma, Abdul Issa, Hassan Mkindai, Erick Yusuph, Idrisa Kilendemo, Nhingo Luzelenga, Sultan Silver na Hussein Mbegu.

    Viungo ni Ismail Likungilo, Razak Mbengelendi, Hassan Kizinga, Hamis Chole, Chenga na Hamisi Barua.

    Washambuliaji ni Luqman Mbalasalu, George Mzungu na Dismas Athanas.

    Viungo wa pembeni ni Abbas Said, Sadam Hussein, Omary Yahaya na Soann Shabani.

    Serengeti Boys ipo Kundi C pamoja na Mali, Angola na Msumbiji. Itacheza mechi yake ya kwanza tarehe 14 Mei dhidi ya Msumbiji katika Uwanja wa Mohammed VI jijini Rabat.

    Mechi ya pili ni tarehe 17 Mei dhidi ya Angola, kabla ya kukamilisha hatua ya makundi dhidi ya Mali tarehe 20 Mei katika Uwanja wa Mohammed VI, Rabat.

    Share.