Timu za Coastal Union ya Tanga, na Singida Black Stars zitacheza mechi ya kwanza ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB (CRDB Federation Cup).

    Mechi hiyo itachezwa tarehe 16 Mei mwaka huu katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Mechi hiyo itaanza kutimua vumbi kuanzia saa 10 kamili jioni.

    Siku hiyo hiyo uga wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa robo fainali ya pili. Mechi hiyo kati ya wenyeji wa uwanja huo JKT Tanzania na Young Africans itafanyika kuanzia saa 12.30 jioni.

    Robo fainali ya tatu (Simba na TRA United), na ya nne kati ya Mashujaa na Azam zitachezwa tarehe 17 Mei mwaka huu.

    Mashujaa itaikabili Azam kuanzia saa 10 kamili jioni katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, wakati ile ya Simba na TRA United itachezwa Meja Jenerali Isamuhyo kuanzia saa 12.30 jioni

    Share.