Twiga Stars yaendeleza ubabe kwa Malawi
Timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars) imeanza vyema mechi za kirafiki za kimataifa k”kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Malawi.
Mechi ya Kalenda ya FIFA ilichezwa tarehe 3 Juni 2026 katika Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
Twiga Stars inayojiandaa na Fainali za WAFCON inatumia mechi hizo kama sehemu ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika Morocco kuanzia Julai 25 hadi Agosti 16 mwaka huu.
Bao pekee la Twiga Stars lilifungwa na Opa Clement dakika ya 48 huku Malawi wakishindwa kupata bao licha ya nafasi nyingi walizopata katika vipindi vyote.
Timu zote mbili zitashiriki katika mashindano ya WAFCON 2026 ambapo Tanzania imepangwa kundi B pamoja na Afrika Kusini, Burkina Faso na Côte d’Ivoire, na Malawi ikipangwa katika kundi C na Nigeria, Zambia na Misri.
Mechi ya pili ya Kalenda ya FIFA kwa timu hizo itafanyika tarehe 6 Juni kwenye uwanja huo huo.

