Tanzanite yatua Yaounde kuikabili Cameroo
Timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imewasili nchini Cameroon kwa ajili ya mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya nne, na ya mwisho itachezwa tarehe 2 Mei 2026 katika Uwanja wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaounde.
Tanzania ilianza harakati za kuwania kufuzu Kombe la Dunia katika raundi ya pili ambapo ilimtoa Angola kwa jumla ya mabao 7-0. Raundi ya tatu ikaiondosha Kenya kwa mikwaju ya penaltı 3-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya marudiano iliyopigwa Azam Complex, Dar es Salaam .
Chini ya uongozi wa Kocha Bakari Shime, wachezaji 23 wamejumuishwa katika kikosi cha Tanzanite kwa ajili ya mechi dhidi ya Cameroon.
Kikosi hicho kinaundwa na Nusrat Jaffar (Fountain Gate Princess), Asha Omary (Simba Queens), Diana Mnally (Yanga Princess), Winfrida Castro (JKT Queens), Ester Maseke (JKT Queens), Lydia Maximilian (JKT Queens), Hasnat Ubamba (FC Masar-Misri), Aliya Fikiri (JKT Queens), Jamila Rajabu (JKT Queens) na Yasinta Mitoga wa JKT Queens, Janeth Matulanga (JKT Queens), Neema Damas (JKT Queens) na Mwanaidi Juma kutoka JKT Queens.
Wengine ni Winfrida Gerald (JKT Queens) Zulfa Makau (JKT Queens), Zawadi Hamis (Simba Queens), Mary Siame (Fountain Gate Princess), Elizabeth Joseph (Simba Queens), Neema Paul (Fountain Gate Princess), Bahati Steven (Bunda Queens), Harrier Juma (Yanga Princess), Veronica Mapunda (Mashujaa Queens) na Christer Basil wa JKT Queens.

