Kahama Madini ya Shinyanga, na Kajuna ya Kigoma zimefuzu kucheza First League msimu wa 2026/2027.
Timu hizo zimepanda daraja baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zilizochezwa tarehe 30 Aprili.
Katika mechi hizo zilizofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Kahama Madini iliifunga Stand FC Masasi mabao 2-1, wakati Kajuna iliiporomoshea Mt. Hanang mabao 8-0.
Timu hizo zitacheza mechi ya fainali kutafuta bingwa wa RCL tarehe 2 Mei kwenye uwanja huo huo. Mechi hiyo itatanguliwa na ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Stand FC Masasi na Mt. Hanang.
Halmashauri ya Kahama iliwahi kuwa na timu ya Ligi Kuu (Kahama United) wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza.

