Shime: Tanzanite bado ina nafasi

    Licha ya timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) kupoteza mechi ya kwanza ya raundi ya nne kuwanka kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon, Kocha Mkuu Bakari Shime amesema bado nafasi ya kufanya vizuri iko wazi.

     

    Mechi ya marudiano kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Poland itachezwa tarehe 10 Mei Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

     

    Tanzanite ilipoteza mechi iliyochezwa tarehe Mei 2 kwa mabao 3-1 katika Uwanja wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaoundé.

     

    Bao pekee la Tanzanite lilifungwa na Winifrida Gerald dakika ya 16 huku mabao matatu ya Cameroon yakifungwa na Maryiam Nyadjou (mawili) na Christiane Meva akihitimisha la tatu kwa mkwaju wa penalti.

     

    Akizungumza baada ya mechi hiyo Kocha Shime alisema: “Mechi bado haijaisha na nafasi ya kufuzu bado tunayo, tutafanyia kazi upungufu ulioonrkana na tutaitumia kikamilifu faida ya kucheza nyumbani.”

    Share.