Simba ni kishindo Kombe la CRDB

    Simba imeingia kwa kishindo nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kuikung’uta TRA United mabao 4-0.

     

    Mechi hiyo ya robo fainali ya michuano hiyo ilifanyika tarehe 17 Mei katika Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam.

     

    Katika hatua ya nusu fainali Simba itakabiliana na Azam FC ambayo tarehe 17 Mei iliing’oa Mashujaa FC kwa bao 1-0 kwenye mechi ya robo fainali iliyochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

     

    Mechi zote za nusu fainali (Yanga v Coastal Union), na Simba v Azam) zitachezwa tarehe 20 Juni katika viwanja vitakavyotangazwa baadaye na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

    Share.