Twiga Stars kambini mechi za FIFA
Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kimeingia kambini Juni 1, 2026 kujiandaa na mechi mbili za Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Twiga Stars itacheza mechi za kirafiki dhidi ya Malawi tarehe 3 na 6 Juni jijini Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji 24 chini ya Kocha Bakari Shime kitatumia mechi hizo kama sehemu ya maandalizi ya Fainali za WAFCON 2026 zitakazofanyika baadae nchini Morocco.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Najiati Abbasi (JKT Queens), Nusra Jafar (Fountain Gate Princess),Janeth Simba (Simba Queens), Enekia Lunyamila (Club Qeuretaro, Mexico), Asha Ramadhani (Simba Queens), Donisia Minja (JKT Queens), Diana Msewa (Trabzonspor, Uturuki), na Ester Mabanza (Yanga Princess).
Opah Clement (Eibar, Hispania), Julietha Tamuwai (FC Juarez, Mexico), Ester Maseke (JKT Queens), Violeth Nicholaus (Palm Hills SC, Misri), Noela Luhala (Mfazalgiris, Uturuki), Anastazia Katunzi (JKT Queens), Suzan Manumbu (Tausi FC), Diana Mnally (Yanga Princess), na Aisha Mnunka (Simba Queens).
Wengine ni Alia Salum (JKT Queens), Elizabeth Mwimi (Simba Queens), Bahati Steven (Bunda Queens), Hasnath Ubamba (FC Masar), Mary Siyame (Fountain Gate Princess), Veronica Mapunda (Mashujaa Queens) na Winfrida Charles (Fontain Gate Princess).

