Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (wa pili kushoto) akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Ligi ya Muungano inayotarajia kuanza Aprili 21 hadi 27, 2026 katika Uwanja wa Amaan Zanzibar

    Kikao hicho kimefanyika Machi 16, 2026 jijini Dar es Salaam kikihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hamza Hassan Juma, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Dkt Riziki Pembe Juma, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na viongozi mbalimbali.

    Ligi hiyo inatarajia kushirikisha timu nane, nne kutoka Tanzania Bra ambazo ni Simba, Yanga, Azam na Singida huku Zanzibar ikishirikisha timu ya Mwembe Makumbi, KVZ, Mafunzo na Mlandege.

    Share.