Timu 16 zimefuzu kucheza raundi ya nne ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB (CRDB Federation Cup) baada ya kushinda mechi za hatua iliyopita.

    Raundi hiyo ilichezwa wikiendi iliyopita na kushirikisha jumla ya timu 32 kutoka madaraja mbalimbali.

    Timu 16 zilizofuzu kucheza raundi ya nne itakayochezwa kati ya tarehe 9 hadi 11 Aprili ni Azam, Coastal Union, na Dodoma Jiji.

    Nyingine ni Fountain Gate, Geita Gold, JKT Tanzania, Mashujaa, Mbeya City, Mbuni, Namungo, Pamba Jiji, Simba, Singida Black Stars, TMA Stars, TRA United, na Yanga.

    Timu zote zilizofuzu hatua hiyo zinatoka katika madaraja mawili; Ligi Kuu ya NBC, na NBC Championship.

    NBC Championship imeingiza timu tatu za Geita Gold, Mbuni na TMA Stars.

    Share.