TFF yapitisha bajeti ya bil 57/-

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepanga kutumia sh. 56,607,000,000 kuendesha shughuli zake kwa mwaka 2026.

    Bajeti hiyo ilipitishwa katika Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) uliofanyika tarehe 28 Februari 2026 Kahama mkoani Shinyanga.

    Akiwasilisha bajeti hiyo, Makamu wa Pili wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango, Athumani Nyamlani alisema pamoja na mambo mengine fedha hizo zitatumika kwenye miradi ya maendeleo.

    Mkutano huo ambao ulifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, pia ulipitisha Taarifa ya Utekelezaji iliyowasilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Oscar Mirambo

    Share.