Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya marekebisho ya Idara zake ikiwemo kuunda tatu mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) uliofanyika tarehe 28 Februari mwaka huu mjini Kahama, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema lengo la mabadiliko hayo ni kuongeza ufanisi.
Ifara tatu mpya zilizoundwa ni Miundombinu, Timu za Taifa, na Ununuzi na Ugavi ambayo awali ilikuwa kitengo.
Wakurugenzi watakaoongoza Idara hizo ni Frank Zomboko (Ununuzi na Ugavi), Salum Madadi (Miundombinu), na Flora Aris (Ukaguzi wa Ndani na Udhibiti).
Wengine ni Boniface Wambura (Sheria, Habari na Masoko), Almasi Kasongo (Timu za Taifa), Hassan Njama (Fedha na Utawala), na Baraka Kizuguto (Mashindano).
Cornel Barnabas yeye ameteuliwa kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).
Uteuzi wa Wakurugenzi hao na CEO ni kuanzia Machi Mosi mwaka huu.

