Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) ipo nchini Misri kwa ajili ya mechi za kirafiki.

    Serengeti Boys imecheza mechi ya kwanza tarehe 14 Machi dhidi ya Misri. Mechi hiyo iliyofanyika katika Kituo cha Ufundi cha Chama cha Mpira wa Miguu nchini Misri (EFA) jijini Cairo ilimalizika kwa suluhu.

    Timu hiyo ambayo ipo nchini humo kwa mwaliko wa EFA itarudiana na Misri tarehe 17 Machi. Timu ya Misri inajiandaa kwa mechi za kufuzu AFCON kwa Kanda ya Kaskazini (UNAF).

    Serengeti Boys ambayo ipo chini ya Kocha Elieneza Nsanganzelu itarejea Dar es Salaam tarehe 18 Machi.

    Mechi za mchujo kwa ajili ya Fainali za AFCON kwa U17 kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) zitachezwa Oktoba mwaka huu nchini Rwanda.

    Tayari Kanda ya Kati (UNIFFAC) imeshapata wawakilishi wake kwenye AFCON ya U17 ambao ni Cameoon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (Congo DR).

    Share.