Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) zitakazokuwa mwenyeji wa mashindano mbalimbali 2026.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA, Jean Sseninde amethibitisha Tanzania itakuwa mwenyeji wa Fainali za CECAFA kwa wanawake chini ya miaka 17 zitakazofanyika Mei 30 hadi Juni 14.
Pia itakuwa mwenyeji wa mashindano ya kufuzu fainali za Kombe la mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 zitakazofanyika Septemba 12 hadi 27, 2026.
Mbali na Tanzania, Rwanda itakuwa mwenyeji wa mashindano manne ya CECAFA ambayo ni Kombe la Kagame (Julai 18 hadi Agosti 9), Mashindano ya CAF kwa Shule za sekondari (Julai 22-25), Mashindano ya kufuzu klabu bingwa kwa wanawake (Agosti 22-06 Septemba) pamoja na kufuzu AFCON kwa vijana chini ya miaka 17 mwezi Oktoba.
Nchi wanachama zinazounda CECAFA) ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Sudan, Sudan Kusini, Somalia, Uganda na Zanzibar.

