Serengeti Queens ya Mara, na TDS ya mkoani Tanga zimepanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake msimu wa 2025/2026.

    Timu hizo zimefanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kwa Wanawake (WRCL) ambayo inafikia tamati tarehe 20 Desemba 2025.

    Ligi hiyo iliyoshirikisha mabingwa kutoka mikoa 16 ilianza tarehe 12 Desemba 2025 jijini Mwanza, na ilichezwa katika viwanja vya Nyamagana, na Alliance.

    Katika nusu fainali ya kwanza TDS iliwazamisha wenyeji Mandozi Queens kwa mabao 2-1.

    Nayo Serengeti Queens ilibidi isubiri hadi dakika ya mwisho kupata ushindi dhidi ya Mpaju Queens ya Mbeya katika nusu fainali ya pili.

    Bao pekee lililoipa Serengeti Queens tiketi ya kupanda daraja, na kucheza fainali katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Nyamagana lilipatikana dakika ya 90 kupitia kwa Amina Karish.

    Mechi ya fainali kati ya TDS na Serengeti Queens ambayo itatoa bingwa wa WRCL itachezwa tarehe 20 Desemba 2025 katika Uwanja wa Nyamagana.

    Ends…

    Share.