Ikiwa ni kipindi cha kalenda ya FIFA, timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) ipo nchini Morocco kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya wenyeji Morocco.

    Mechi zitachezwa tarehe 13 Aprili, wakati ya pili itapigwa Aprili 18.

    Tanzania na Morocco zitacheza Fainali za WAFCON Julai mwaka huu, ambapo mechi hizo mbili ni sehemu ya maandalizi.

    Mechi ya kwanza itaanza saa 5:00, na itafanyika kwenye Uwanja wa Moulay El Hassan.

    Wachezaji wanaounda kikosi cha Twiga Stars ni Najiat Abbas, Asha Mrisho, Zulfa Makau, Enekia Kasonga, Lidya Kabambo, Donisia Minja, Anastazia Katunzi, Ester Maseke, Julitha Singano, Winfrida Castor, Noela Luhala na Janet Pangamwene.

    Wengine ni Opah Clement, Susan Adam, Aisha Juma, Hasnath Ubamba, Elizabeth Joseph, Joyce Lema, Clara Luvanga, Winfrida Gerald, Jamila Rajabu na Neema Paul, Alia Fikiri, Yasinta Mitoga, Violeth Nicholas na Diana Mnaly.

    Share.