Kajuna mabingwa RCL 202
Timu ya Kajuna FC ya Kigoma imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kajuna ilipata ushindi huo dhidi ya Kahama Madini ya Shinyanga, katika mechi ya fainali iliyochezwa tarehe 2 Mei kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Mabao yote ya Kajuna yalifungwa kipindi cha pili kupitia kwa Yusuph Kikoko (dakika ya 60), na Abasi Haruna (dakika ya 66).
Nayo Mt. Hanang ya Manyara iliifunga Stand FC Masasi ya Mtwara bao 1-0 katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.
Bao la washindi lilifungwa dakika ya 72 kupitia kwa John Urasa.

