Mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (WPL) mzunguko wa 5 zinazoanza kutimua vumbi Desemba 27, zitaamuliwa na mbabe mmoja kutoka kwenye mechi nambari 30 kati ya watani Yanga Princess na Simba Queens.Mechi hiyo ya kufunga mzunguko huo itapigwa Desemba 28, 2025 Azam Complex Chamazi kuanzia saa 12:00 jioni, binti mfalme Yanga Princess wakiwakaribisha Malkia wa Mwitu Simba Queens.Wakizingumzia mechi hiyo, makocha wa timu zote mbili wamejinasibu kuonesha ukubwa wao kwa kubeba pointi zote tatu kila mmoja.Kocha wa Queens, Mussa Mgosi alisema timu yake imejiandaa vizuri na wana kila sababu ya kushinda licha ya kuwakosa wachezaji takribani saba ambao ni majeruhi.Alisema hayupo tayari kupoteza mbele ya Kocha Edna Lema kwa kuwa kikosi chake ni bora zaidi, hivyo ni jukumu la wachezaji kuonesha kwalichofanyia kazi uwanja wa mazoezi.Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake wa Queens, Vivian Corazone alisema wamejipanga kuchukua pointi zote tatu kwenye mechi hiyo.Kwa upande wa Yanga Princess, Kocha Lema alisema wanawaheshimu wapinzani wao, lakini lengo lao kubwa ni pointi tatu.Amewataka washabiki wao kufika kwa wingi Azam Complex Chamazi kwa ajili ya kuwaunga mkono na kusisitiza dakika 90 zitaamua timu bora.Nahodha wa Princess, Irene Kisisa alisema ushindi kwenye kila mechi ndio kitu pekee wanachokitaka wao, hivyo hakuna cha kuwarudisha nyuma.Queens na Princess ndizo timu pekee ambazo zimeshinda mechi zao zote hadi sasa tangu msimu wa 2025/2026 uanze.Ends…
Saturday, March 7
Trending
- TFF yapitisha bajeti ya bil 57/-
- TFF yarekebisha muundo wa idara zake
- AGM yapitisha Taarifa ya Utekelezaji
- RC Shinyanga mgeni rasmi Mkutano Mkuu wa TFF
- Twiga yajinoa Misri kwa ajili ya WAFCON 2026
- Gamondi kuiongoza Stars AFCON 2027
- Tanzanite yachanja mbuga Kombe la Dunia 2026
- Futsal yaanza upyaa ugenini

