Timu hiyo ambayo tayari imewasili nchini Ivory Coast, imeendelea na matayarisho yake ya mwisho kuisaka tiketi ya kwenda kushiriki Fainali za Afrika (AFCON 2026).

    Ni baada ya kupata ushindi wa mabao 7-3 kwenye mechi ya nyumbani iliyochezwa Februari 3, 2026 Uwanja wa Amaan Indoor, Zanzibar.

    Timu ya Taifa ya Wanaume ya Futsal imeanza hesabu mpya za mechi ya ugenini, ya marudiano dhidi ya Ivory Coast inayochezwa Februari 7, 2026.

    Akizungumzia matayarisho mechi hiyo, Kocha Mkuu Curtis Reid alisema kikosi chake kipo tayari na kuwa wamekuwa wakifanyia masahihisho makosa kadhaa yaliyojitokeza kwenye mechi ya nyumbani ili wapate ushindi mwingine.

    Alisema kuwa hakuna majeruhi kwenye kikosi hicho na badala yake kila mchezaji yupo tayari.

    Share.