Timu ya Simba Queens imeendeleza ubabe Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) baada ya kubeba pointi tatu nyingine mbele ya watani wake Yanga Princess kwenye mchezo uliomalizika kwa ushindi wa mabao 2-0.Mechi hiyo iliyochezwa Desemba 28, 2024 Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam ulivutia washabiki wengi kwa kasi yake huku timu zote zikionesha dhamira ya kushinda.Hata hivyo uongozi wa mechi ulianza kutwaliwa na Simba Queens waliotumia uzoefu wao vizuri kuwasumbua walinzi wa Yanga Princess na kufanikiwa kuandika bao la kwanza dakika ya 36 kupitia mshambuliaji wao Jentrix Shikangwa.Kipindi cha pili timu zote zilirejea na kasi ileile, wakati Yanga Princess ikitafuta bao la kusawazisha, Simba Queens waliendelea kuimarisha ulinzi hadi walipoongeza bao la pili.Kwa matokeo hayo Simba Queens imefanikiwa kupanda kileleni na kuongoza ligi ikiwa ndio timu pekee ambayo haijadondosha alama yoyote hadi raundi hiyo, ikifikisha pointi 15.Matokeo ya mechi nyingine ni; Geita Queens 3-1 Ruangwa Queens, Tausi FC 1-2 Alliance Girls, Bunda Queens 1-1 Ceassia Queens, Bilo 0-3 Fountain Gate Princess na JKT Queens 6-0 Mashujaa Queens.Ends…
Saturday, March 7
Trending
- TFF yapitisha bajeti ya bil 57/-
- TFF yarekebisha muundo wa idara zake
- AGM yapitisha Taarifa ya Utekelezaji
- RC Shinyanga mgeni rasmi Mkutano Mkuu wa TFF
- Twiga yajinoa Misri kwa ajili ya WAFCON 2026
- Gamondi kuiongoza Stars AFCON 2027
- Tanzanite yachanja mbuga Kombe la Dunia 2026
- Futsal yaanza upyaa ugenini

