Kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kimewasili leo nchini Morocco, tayari kwa ajili ya Fainali za Afrika (AFCON) zitakazoanza Jumapili, tarehe 21 Desemba 2025.
Stars imewasili nchini humo ikitokea Misri ambapo iliweka kambi yake ya maandalizi chini ya Kocha Miguel Gamondi.
Raia huyo wa Argentina anakiongoza kikosi hicho ambapo katika Fainali hizo kimepangwa kundi C pamoja na Nigeria, Tunisia, na Uganda.
Stars yenye kikosi cha wachezaji 28 itacheza mechi yake ya kwanza Jumanne, Desemba 23 dhidi ya mabingwa wa mwaka 1980, Nigeria.
Mechi ya pili katika hatua hiyo ya makundi itakuwa Desemba 27 dhidi ya Uganda, wakati ya mwisho ni Desemba 30 itakapoikabili Tunisia.
Hii ni mara ya nne kwa Tanzania kucheza fainali hizo. Ilishiriki fainali za 1980 nchini Nigeria, 2019 (Misri), na 2023 (Cote d’Ivoire).
Ends…

