Tanzania (Taifa Stars) imeanza vibaya Fainali za 35 za Kombe la Afrika (AFCON) zinazofanyika nchini Morocco.

Ikicheza mechi yake ya kwanza katika Fainali hizo leo mjini Fes, Stars imepoteza mbele ya Nigeria (Super Eagles) kwa mabao 2-1.
Stars inayonolewa na Manuel Gamondi, raia wa Argentina ilitanguliwa kipindi cha kwanza kwa bao 1-0.
Ilisawazisha dakika ya 50 kupitia kwa mshambuliaji Charles M’mombwa. Bao hilo liliongeza kasi ya mchezo huo wa Kundi C.

Nigeria wakiongozwa na Victor Osimhen walifanikiwa kuondoka na pointi zote tatu baada ya kupata bao la pili katika kipindi cha pili.
Waliounda kikosi cha Stars katika mechi hiyo ni Zuberi Foba, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Ibrahim Hamad, Bakari Mwamnyeto, Novatus Dismas, Alphonce Mabula, Simon Msuva, Charles M’mombwa, Mbwana Samata, na Tarryn Allarakhia.

Stars itacheza mechi yake ya pili Desemba 27 dhidi ya Uganda, na itahitimisha mechi za makundi Desemba 30 kwa kuikabili Tunisia.

Ends…

