Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Miguel Gamondi amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa hatua ya 16 bora wa mashindano ya Afrika (AFCON) dhidi ya Morocco.Mchezo huo utachezwa Januari 4, 2026 katika uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Rabat kuanzia saa moja kamili usiku.Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo, Kocha Gamondi alisema: “Morocco ni timu kubwa na ni tofauti na timu tilizocheza nazo hatua ya makundi.“Wana faida ya kuwa na mashabiki wengi na wanahamasisha timu kufanya vizuri. Ninafahamu nini cha kufanya kimbinu ili timu icheze vizuri”.Nahodha wa Stars, Mbwana Samatta alisema amecheza na Morocco mara nyingi, na ni timu ambayo huwa inabadilika kulingana na aina ya mashindano.Aliongeza kuwa Morocco ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wazuri. Wamewaona wakicheza katika hatua ya makundi na wamejiandaa kuwakabili kwa aina yoyote ya uchezaji.Tanzania na Morocco ni miongoni mwa nchi 16 za Afrika zilizofuzu hatua ya mtoano katika mashindano ya Afrika (AFCON). Nyingine ni Nigeria, Tunisia, DR Congo, Nigeria, Senegal, Algeria, Burkina Faso, Mali, Afrika Kusini, Misri, Benin, Ivory Coast na Msumbiji.
Saturday, March 7
Trending
- TFF yapitisha bajeti ya bil 57/-
- TFF yarekebisha muundo wa idara zake
- AGM yapitisha Taarifa ya Utekelezaji
- RC Shinyanga mgeni rasmi Mkutano Mkuu wa TFF
- Twiga yajinoa Misri kwa ajili ya WAFCON 2026
- Gamondi kuiongoza Stars AFCON 2027
- Tanzanite yachanja mbuga Kombe la Dunia 2026
- Futsal yaanza upyaa ugenini

