Serengeti Girls yatua Jo’burg kuivaa Bantwana

    Ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya mechi ya marudiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini (Bantwana) kuchezwa Mei 31, kikosi cha Serengeti Girls kimewasili jijini Johannesburg tayari kwa mechi hiyo.

    Mechi hiyo ya mkondo wa pili raundi ya tatu itachezwa Uwanja wa Lucas Moripe uliopo katika mji wa Pretoria.

    Serengeti Girls ilipoteza mechi ya kwanza kwa mabao 2-0 kisowani Zanzibar, hivyo itahitaji ushindi wa kuanzia mabao 3-0 ili isonge mbele katika raundi ya nne na ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia kwa mwaka huu.

    Timu 20 kati ya 24 zimefuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia kwa wanawale chini ya miaka 17 zitakazofanyika Morocco, hivyo zimesalia timu nne pekee kutoka ukanda wa Afrika (CAF) ili kutimiza idadi ya timu 24.

    Timu zilizofuzu ni Morocco, New Zealand, Ujerumani, Argentina, Korea, Puerto Rico, Poland, Canada, Brazil, Norway, Japan, Ufaransa, Venezuela, Marekani, Samoa, Hispania, Mexico, Australia, China na Chile.

    Share.