Young Africans kukipiga na TMA Stars 16 Bora CRDB Federation Cup

    Wakati timu mbalimbali zikiendelea kuchanga karata zao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB Benki, timu ya Young Africans inatarajia kushuka dimbani dhidi ya TMA United kwenye hatua hiyo.

    Mchezo huo utakao watambulisha Young Africans kama wenyeji unatarajiwa kupigwa majira ya saa 12:30 jioni katika dimba la KMC.

    Akizungumza kuelekea mchezo huo kocha wa TMA Stars Omary Matwiko alisema kikosi chake kimejiandaa vizuri na kwamba kipo tayari kuwakabili wapinzani wao ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

    Ameeleza kuwa watauendea mchezo huo kwa kuwaheshimu Young Africans kutokana na mafanikio yao, huku wakiwa na lengo kuu la kufanya vizuri zaidi kupitia mchezo huo.

    Kwa upande wa mchezaji wa TMA Stars Wilson Chigombo, alisema wachezaji wamejiandaa kikamilifu kwa mchezo huo mgumu, wakilenga kupata matokeo mazuri huku wakitambua ubora wa wapinzani wao.

    Naye kocha wa Yanga, Pedro Gonçalves, alisema timu yake ipo tayari kwa mchezo huo na wanaheshimu wapinzani wao, huku wakilenga kuendeleza ubora wao kama mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

    Kwa niaba ya wachezaji, Allan Okello alisema maandalizi yamekamilika na wapo tayari kwa mchezo huo, huku dhamira yao kuu ikilenga kupata ushindi na kusonga mbele katika hatua inayofuata.

    Hata hivyo wakati nyasi za KMC zikiumana kwa mchezo huo, mtanange mwingine utapigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga majira ya saa 10:00 jioni; wanamangushi Coastal Union wakiwakaribisha Pamba jiji kutokea Mwanza.

    Share.