Serengeti Boys yaanza AFCON kwa kishindo
Timu ya Taifa ya Wavulana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imeanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2026 kwa kuichapa Msumbiji mabao 3-0.
Mechi hiyo ya kwanza kwa Serengeti Boys ilifanyika tarehe 14 Mei katika Kituo cha Ufundi cha Mohammed VI saa 1 usiku.
Serengeti Boys ilihitimisha kipindi cha kwanza ikiongoza mabao 2-0.
Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Dismas Athanas, na Razaki Mbegelendi na beki Paschal Miambo wa Msumbiji alijifunga.
Akizungumza baada ya dakika 90, mchezaji bora wa mechi jiyo Issa Mussa Chole alisema juhudi zao sambamba na kazi kubwa ya benchi la ufundi ndivyo vilivyowapa matokeo.
“Niwapongeze wachezaji wenzangu sambamba na benchi la ufundi kuwasoma wapinzani wetu, na hatimae tulifanikiwa kutumia udhaifu wao na tumepata ushindi,” alisema Chole.
Serengeti Boys ambayo ipo Kundi C, katika hiyo imebakiza mechi dhidi ya Mali na Angola.

