Tanzania yapangiwa kundi CECAFA U17 Wanawake

    Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetaja makundi ya michuano ya wanawake chini ya miaka 17.

    Tanzania (Serengeti Girls) imepangwa kundi A la michuano hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 23 Juni mwaka huu.

    Timu nyingine za kundi A katika michuano hiyo itakayoshirikisha jumla ya mataifa saba ni Kenya, Somalia, na Sudan.

    Kundi B linaundwa na mataifa ya Djibouti, Sudan Kusini, na Uganda.

    Somalia na Sudan zinashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza. Mechi zitachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.

    Share.