Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) yanayoendelea barani Afrika yameibua fursa kubwa kwa wafanyabiashara wa jezi nchini, hususan visiwani Zanzibar. Mwitikio mkubwa wa mashabiki wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, umesababisha ongezeko la mahitaji ya jezi, bendera na bidhaa nyingine za michezo.

    Wakizungumza na Mwananchi Digital, baadhi ya wafanyabiashara wa michezo wamesema kuwa tangu kuanza kwa michuano hiyo, mauzo yao yameongezeka kwa kiwango kikubwa. Wateja wengi wameripotiwa kununua jezi za Taifa Stars kama ishara ya kuonyesha mshikamano na timu yao katika safari ya kuwania ubingwa wa CHAN.

    Bi Asha Suleiman, mfanyabiashara wa jezi eneo la Darajani, amesema:

    “Hii ni fursa kwetu. Mashabiki wanakuja na ari kubwa, wanataka kuvaa jezi mpya za Stars kila mechi. Kila siku tunauza zaidi ya tulivyotarajia.”

    Vilevile, wauzaji wameeleza kuwa mahitaji hayajabaki tu kwenye jezi bali yameenea hadi kwenye bidhaa kama kofia, skafu, na bendera za Taifa Stars. Bidhaa hizi zimekuwa zikiuzwa kwa kasi kwenye maeneo ya biashara na hata viwanja vya michezo.

     

    Share.