Mechi ya Fainali za Kombe la Afrika (AFCON) 2025 kati ya Tanzania na Uganda iliyochezwa Desemba 27 imemalizika kwa sare huku akichomoza mshambuliaji Simon Msuva.Timu hizo zilimaliza mechi hiyo ya Kundi C iliyochezwa Rabat, Morocco kwa sare ya bao 1-1, huku bao la Tanzania likifungwa na Msuva dakika ya 59.Msuva ameifunga Uganda kwa mara ya nne katika mechi tano zilizopita za timu hizo. Ukiondoa mechi hiyo ya AFCON ambapo bao la Uganda lilifungwa na Uchechukwu Ikpeazu dakika ya 80, Msuva pia ameifunga katika mechi nyingine tatu.Aliifunga Uganda katika mechi mbili za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za AFCON, na mechi ya kirafiki ya Kalenda ya FIFA.Taifa Stars ambayo ipo chini ya Kocha Miguel Gamondi ilipoteza mechi ya kwanza ya Fainali hizo kwa mabao 2-1 mbele ya Nigeria.Stars itacheza mechi ya mwisho ya hatua ya makundi ya fainali hizo za 35 dhidi ya Tunisia, Desemba 30, 2025.Ends …

    Share.