Tanzania imeandika historia kwenye Fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza kucheza raundi ya mtoano.Timu ya Taifa (Taifa Stars) imefuzu hatua hiyo baada ya Desemba 30, 2025 kutoka sare ya bao 1-1 na Tunisia katika mechi yao ya mwisho ya Kundi C.Bao la Stars lililoipa pointi hiyo moja na kufuzu kama mshindwa bora (best looser) katika mechi hiyo iliyochezwa Rabat, Morocco lilifungwa dakika ya 64 kupitia kwa Feisal Salum.

    Tunisia ndiyo ilitangulia kupata bao katika mechi hiyo lilifungwa kipindi cha kwanza. Nigeria na Tunisia kutoka C pia zimefuzu kucheza raund ya mtoano- 16 bora.Mechi za 16 bora zitachezwa kati ya tarehe 3 hadi 6 Januari 2026.Stars ambayo inafundishwa na Kocha Miguel Gamondi imemaliza hatua ya makundi ikiwa na pointi mbili baada kupata sare mbili, na kupoteza mechi moja mbele ya Nigeria.

    Kikosi cha Stars kilichoanza katika mechi hiyo dhidi ya Tunisia kiliundwa na;Hussein Masalanga, Haji Mnoga, Mohamed Hussein, Dickson Job, Ibrahim Hamad, Bakari Mwamnyeto, Novatus Damian, Alphonce Mabula, Feisal Salum, Mbwana Samata, na Simon Msuva.

    Share.