Mkutano Mkuu wa Kawaida wa 20 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika tarehe 28 Februari 2026 katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu huo utakaohudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, vyama shirikishi na klabu za Ligi Kuu ya NBC atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Mboni Mhita.
Wajumbe wa Mkutano huo utakaoongozwa na Rais wa TFF, Wallace Karia watajadili ajenda mbalimbali zinazohusu maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Lakini pia kutakuwa na Uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF anayewakilisha Kanda Namba Moja.
Mbali ya wajumbe, lakini pia kutakiwa wageni kutoka FIFA, na waalikwa wengine mbalimbali wakiwemo wadhamini.
Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha Kawaida cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika tarehe 27 Februari 2026.

