Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) 2026 hatua ya makundi imeanza kutimua vumbi leo Machi 13, 2026 ikijumuisha timu 28 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

    Timu hizo 28 zimegawanywa katika makundi manne ambapo kila kundi lina timu saba zinazocheza ligi ya mkondo mmoja katika vituo vinne tofauti.

    Mechi zilizochezwa leo kwa upande wa kundi A katika kituo cha Kigoma ilikua kati ya Kijuna FC dhidi ya Kyela Talents, na mchezo huo ulimalizika kwa Kajuna FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika dimba la Lake Tanganyika.

    Kundi B katika kituo cha Geita , timu ya Geita Institute ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kahama Madini katika Uwanja wa Waja Boys, huku kundi C katika kituo cha Babati, Manyara United aliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Hai United katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa.

    Mchezo wa kundi D kituo cha Bagamoyo ulimalizika kwa timu ya Bagamoyo Sugar kupoteza mbele ya Lindi Soccer Academy kwa mabao 3-0 katika Uwanja wa Mwanakalenge.

    Share.