What's Hot

    Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachocheza mechi mbili za FIFA Series 2026 zitakazofanyika Kigali, Rwanda kuanzia Machi 26-31, 2026.

    Nchi nane zitashiriki katika mechi hizo zikigawanywa katika makundi mawili. Kundi A linajumuisha timu mwenyeji Rwanda, Kenya, Estonia pamoja na Grenada huku kundi B likiwa na timu ya Tanzania, Aruba, Macau na Liechtenstein.

    Wachezaji waliojumuishwa katika kikosi ni Aishi Manula (Azam FC), Yona Amos (Pamba Jiji), Zuberi Foba (Azam FC), Mohamed Mussa (Mashujaa FC), Twalib Nuru (Azam FC), Bakari Msimu (Coastal Union), Elias Lameck (Azam FC), Haji Mnoga (Salford City, Uingereza), Nickson Kibabage (Simba SC), Bakari Mwamnyeto (Young Africans), Mohamed Hussein (Young Africans) na Ibrahim Abdulla (Young Africans).

    Wengine ni Yusuf Kagoma (Simba SC), Kelvin Nashon (Pamba Jiji), Mudathir Yahaya (Young Africans), Novatus Dismas (Goztepe FC, Uturuki), Alphonce Mabula (Shamakhi, Azerbaijan), na Feisal Salum (Azam FC).

    Katika kikosi hicho pia wamejumuishwa Simon Msuva (Al-Talaba, Iraq), Kelvin John (Aalborg BK, Denmark), Idd Suleiman (Azam FC), Charles M’mombwa (Floriana FC, Malta), Tarryn Allarakhia (Rochdale AFC, Uingereza), Paul Peter (JKT Tanzania) na Suleiman Mwalimu (Simba SC)

    Stars wataingia kambini Machi 23, 2026 kujiandaa na mechi hizo za FIFA Series.

    Share.