Timu ya Taifa “Taifa Stars” kupitia kocha Mkuu wake Hemedi Suleiman Morocco imeweka wazi kuwa timu imejipanga vilivyo kuuendea mchezo wa robo fainali dhidi ya morroco Augost 22 Kwa Mkapa.

    Mchezo huo wa kwanza kwa hatua hiyo ya robo fainal kwa Stars kwenye michuano ya CHAN 2024 unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 2:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo Mashujaa hao watashuka dimban kuisaka tiketi ya kwenda katika hatua inayofua ya nusu fainail.

    Akizungumzia maandalizi kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Agosti 21,2025 Benjamin Mkapa kocha wa Taifa Stars Hemed Suleiman Morocco alisema kikosi chake kipo tayari kuhakikisha kinapata matokeo mazuri kwenye mechi ya Agosti 22, 2025 dhidi ya Morocco.

    Morocco alisema awali dhamira ilikuwa ni kuvuka hatua ya makundi, ambapo baada ya kufanikiwa, kwa sasa wanalenga kusonga mbele zaidi hata kubeba Ubingwa huo ikibidi.

    “Tangu tulipoanza maandalizi ya mashindano haya, tulijiwekea malengo mawili makubwa – kushinda kila mechi na kumaliza tukiwa vinara wa kundi. Hatujapanga kupoteza hata mchezo mmoja, na kesho tunataka kuthibitisha hilo.Kila mchezo tumekutana na upinzani mkali, lakini wachezaji wameonesha nidhamu ya hali ya juu na ari kubwa ya kushinda. Hii ndiyo sababu tunaamini tunastahili tulipo sasa”. Alisema Morocco.

    Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa mashabiki wamekuwa silaha muhimu kwa mafanikio ya kikosi hicho huku akisisitiza wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo huo kwa ajili ya kuendelea kuisapoti timu.

    Ikumbukwe hii ndio mara ya kwanza kwa timu ya Taifa Stars kutinga hatua ya robo Fainali, ikiweka na rekodi zaidi ya kumaliza hatua ya makundi wakiwa vinara.

    Share.