Timu ya Young Africans imeanza vyema mwaka 2026 kwa kutwaa Kombe la Mapinduzi, Januari 13 kwa ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Azam FC katika Uwanja wa Gombani ksiwani Pemba.Mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkali, kila timu kuonesha nidhamu ya hali ya juu kiuchezaji ilitamatisha dakika 90 za kwa suluhu. Kwa kipindi hicho makipa wa timu zote (Aishi Manula, Azam) na Abdutwalib Msheri wa Young Africans ndiyo waliong’ara kwa kuzuia mipira ya hatari.Hatimaye, mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penalti. Young Africans walifunga penalti zote tano wakati wapinzani wao Azam walipoteza penalti moja iliyopigwa na Immanuel Mwanengo.Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge aliwapongeza wachezaji wake kwa kujituma na kukubali kuwa bahati haikuwa upande wao.”Nawapongeza wachezaji wangu kwa kupambana na kutoruhusu bao kwa dakika zote mpaka za nyongeza. Tumepoteza penalti, hivyo bahati haikuwa upande wetu kwa leo,” alisema Ibenge.Naye Kocha Mkuu wa Young Africans, Pedro Goncalves aliwapongeza wachezaji wake na kusifu upinzani walioonesha Azam FC.”Nawapongeza wachezaji wamepambana licha ya upinzani mkubwa walioonesha Azam. Wameonesha wapi natakiwa kufanya kazi zaidi kwenye kikosi changu,” alisema Goncalves.Young Africans walitwaa ubingwa huo mwaka 2007 na 2021, huku Kombe la mwaka 2026 likifanya timu hiyo kufikisha makombe matatu ya Mapinduzi.
Friday, May 1
Trending
- Kahama, Kajuna zapanda daraja
- Tanzanite yatua Yaounde kuikabili Cameroon
- Nne zafuzu nusu fainali RCL
- Coastal, Singida robo ya kwanza Kombe la CRDB
- BetaTQ mshirika wa TFF kwenye data
- Serengeti Girls kuikabili Afrika Kusini Kombe la Dunia
- Kocha ‘afagilia’ mechi za kujipima Twiga Stars
- Ratiba robo fainali Kombe la CRDB hadharani

