Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliofanyika tarehe 28 Februari 2026 umepitisha Taarifa ya Utekelezaji ya mwaka 2025.

    Taarifa hiyo ya Utekelezaji iliwasilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Oscar Mirambo katika Mkutano huo Mkuu wa Kawaida wa 20 uliofanyika Ukumbi wa Malex mjini Kahama, mkoani Shinyanga.

    Mkutano huo ulioongozwa na Rais wa TFF, Wallace Karia pia ulipitisha taarifa mbalimbali ikiwemo hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2024, na bajeti ya 2026.

    Pia ulifanyika Uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF anayewakilisha Kanda Namba Moja. Lameck Nyambaya ambaye hakuwa na mpinzani alichaguliwa kujaza nafasi hiyo.

    Share.