Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema amesema ushindi walioupata dhidi ya JKT Queens umewarejesha kwenye mbio za Ubingwa.

    Lema ametoa kauli hiyo baada ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Wanawake iliyochezwa Azam Complex, Januari 18, 2026 kumalizika kwa Yanga Princess kushinda bao 1-0.

    Mechi hiyo ya kuvutia ilikuwa mgumu kwa pande zote, timu zote zilipata nafasi chache za kushambulia hali iliyosababisha timu hizo kwenda mapumziko zikiwa suluhu..

    Mambo yalibadilika kipindi cha pili baada ya Yanga Princess kupata bao dakika ya 83.

    Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha Lema alisema ilikuwa kati ya mechi bora za Ligi kutokana na ugumu ulioonekana kwa timu zote.

    “Hivi ndivyo mechi kubwa huwa zinachezwa, matokea haya yanaturejesha kwenye mbio za kuwania uningwa baada ya kupoteza mechi yetu dhidi ya Simba Queens,” alisema.

    Kwa upande wa Kocha Mkuu wa JKT Queens, Juma Kessy matokeo hayo sio mazuri kwa upande wao.

    Mechi hiyo ilikuwa ni mwendelezo wa Ligi hiyo kwa mzunguko wa 9 ambapo mechi nyingine zilipigwa pia kwenye viwanja mbalimbali.

    Matokeo ya mechi nyingine ni; Mashujaa Queens 1-2 Simba Queens, Tausi FC 1-0 Geita Queens, Ruangwa Queens 0-2 Alliance, Bilo 0-3 Ceasiaa Queens na Fountain Gate Princess 2-0 Bunda Queens.

    Share.