Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 15 inaendelea na maandalizi kwa ajili ya Fainali za African Schools zinazotarajiwa kufanyika Machi mwaka huu.Tayari hiyo iliyopo kambini Kituo cha Ufundi cha TFF Mnyanjani, Tanga imecheza mechi mbili za kirafiki za kushinda zote.Katika maandalizi yake chini ya Kocha Boniface Pawasa, kikosi hicho kinaendelewa kuboreshwa kabla ya kwenda kwenye Fainali hizo zitakazofanyika nchini Nigeria.

    Pia Kocha Pawasa alisema timu yake inatarajia kushiriki mashindano mengine ya kirafiki jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 20 ikiwa ni sehemu ya maandalizi.“Tutakuwa na mashindano maalum yanayoitwa Building Capacity yatakayoshirikisha timu nne (Young Africans U17, Simba SC U17, Azam FC U17 na TDS U15).“Lengo kubwa ni kuandaa zaidi timu yetu kwa kupata mechi nyingi. Lakini pia tutatumia nafasi hiyo kuongezea baadhi ya wachezaji watakaounda kikosi chetu cha mwisho,”alisema Pawasa.Alisema hadi sasa kikosi kina wachezaji 21 waliopatikana kwenye programu ya kusaka vipaji iliyofanyika maeneo mbalimbali nchini.Fainali za ASFC zitafanyika kwa mara ya tatu ambapo Tanzania ilifanikiwa kutwaa ubingwa mara mbili.

    Share.